NEW UPDATES

Mh temba: Atoboa siri ya kuvunjika kwa kundi la yamoto Band

Mh Temba: Atoboa siri ya kuvunjikwa kwa kundi la Yamoto Band

Dar es Salaam. Mashabiki wengi wa muziki nchini bado wapo katika sintofahamu juu ya sababu ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto Band, mwanamuziki Mh Temba ametoboa siri hiyo.

Tangu kusambaratika kwa kundi hilo mara kadhaa wanamuziki hao wamekuwa wakikanusha, lakini mwendo unaoendelea ni kuwa hali katika kundi hilo si shwari tena.

Katika moja ya mahojiano Mh Temba alisema kusambaratika kwa kundi hilo kumetokana na fedha kuingilia kati na hivyo kusababisha kila mmoja kutaka kuwa na sauti yake.

“Mimi nakupa mfano hawa Yamoto, utaona labda kuna mtu anasimamia msanii fulani, mbona hakumchukua mwanzo wakati hajulikani kabla hatujamkuza na kuwa superstar,” amesema Temba.

“Huyo mtu kama ana uwezo kwanini asingekuwa na vipaji vyake, wewe unaona tayari nuru inang’aa unaenda kuchomoa pale,” ameongeza.

Kundi la Yamoto liliundwa na Aslay, Maromboso, Beka Flavour na Enock Bella ambao kwa sasa kila mmoja anafanya kazi peke yake.


No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link