NEW UPDATES

KINGA NA MATIBABU YA CORANA VIRUS

CORONA VIRUS ni virusi vinavyotokea kwenye familia iitwayo Coronaviridae, na vimepewa jina hilo kutokana na muonekano wake wa "Crown-like projection" chini ya light microscope.

Virusi hivi vinaathiri moja kwa moja mfumo wa upumuaji wa binadamu ambapo huweza kupelekea matatizo kwenye mfumo wa upumuaji (Respiratory Tract Infection), especially, "Common Cold"

Pia unatajwa kama ni ugonjwa wa pili unaosababisha atypical pneumonia, baada ya ule unaosababishwa na Rhinovirus

Inasemekana huko China, kwenye mji wa Wuhan, kati ya watu 10, watu 5 wanaweza kukutwa na maambukizi ya hivi virusi.

CHANZO
- Ugonjwa huu unaosababishwa na virusi aina ya coronavirus na unaaminika kuanzia China kwenye mji wa Wuhan.

JINSI UGONJWA UNAVYOSAMBAA (Mode of Transmittion)
Mwanzoni ilikuwa inaaminika kuwa ugonjwa huo umetokea kwa wanyama walioathirika na hivyo virusi (Mfano, Ngamia na Ng'ombe) lakini baadae ikaja kufahamika zaidi kuwa ugonjwa umejikita kwa mtu na mtu (person-to-person transimittion) kupitia:

1. Air transmission (Infective air droplets). Kwa mfano, muathirika anapokohoa ni rahisi kupata vimelea kama ukiwa karibu kwa njia ya hewa.

2. Kugusana moja kwa moja (Direct Contact) na muathirika

DALILI
• Homa (Fever)
• Kikohozi cha mara kwa mara (Cough)
• Kuumwa kichwa (Headache)
• Pia inaweza kupelekea Shortness of breath

KINGA NA MATIBABU


1. KINGA (Vaccination)

Mpaka sasa, hakuna chanjo iliyogundulika kwa ajili ya kutibu hili tatizo. Bado wanasayansi wanaendelea kulifanyia kazi.

Ilikuwa inaaminika kuwa huenda chanjo kwa ajili ya mafua (Flu Vaccine) ingeweza kusaidia kwa kuwa zote zinapelekea Common Cold, lakini kwa bahati mbaya kinga hiyo haijaweza kusababisha tofauti yoyote.

2. MATIBABU

Kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya virusi. Hakuna matibabu sahihi ya virusi.
Kwahiyo dawa zitatolewa kutokana na dalili zitakazojitokeza.

NAMNA YA KUZUIA/KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI
- Kama ni muathirika unashauriwa kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi kuepusha kusambaza vimelea

- Osha mikono yako mara kwa mara kwa sabuni na maji yanayotiririka

- Epuka kugusana na mtu alieathirika

- Epuka kujifanyanga kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu (Overcrowded Areas)

- Vaa viziba uso (Mask). Huwenda vikasaidia kupunguza maambukizi

- Wahi kwenye vituo vya afya mapema tu unapoona dalili zinaanza kujitokeza.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link