NEW UPDATES

Njia 5 za kufufua mahusiano yaliyokufa.

Njia 5 za kufufua mahusiano yaliyokufa
#Bakihotnews
Katika nyakati hizi tunazoishi wakati huu, mambo yamebadilika sana. watu wengi wako bize kutafuta fedha na kutengeneza maisha yao ili yawe bora.
Jambo hili linafanya watu kuutumia muda mwingi katika shighuli ambazo zinawaingizia kipato na wengine hufikia mpaka hatua ya kuwasahau wapenzi wao ama familia zao.
Jambo hili limechangia sana kuvunjika kwa mahusiano ama yaliyopo kukosa uhai.
Je penzi lako limedhoofika? basi usipate tabu kufikiria ni namna gani unaweza kulifanya lenye afya tena.
Hizi hapa ni baadhi ya mbinu unazoweza kuzitumia kulihuisha tena penzi lililokosa afya.
Tenga muda wa kukaa na mpenzi wako
Jitahidi kadri ya uwezo wako kutenga muda wa ofisi na muda wa nyumbani. Muda wa kazi, fanya mambo yanayohusu ofisi, kamwe usilete mambo ya kazini nyumbani. Unaporudi nyumbani hakikisha kuwa muda ule unaokuwepo unatumia mudawako na mpenzi wako au mkeo na watoto kama umeoa. Muda huu utakaoutumia pamoja na familia yako, utasaidia sana kulifufua penzi lenu ambalo liko katika hatari ya kutoweka kabisa.
Jifunze kusifia na kutoa pongezi.
Hakuna binadamu asiyependa kusifiwa. Kila mmoja wetu hupenda kupongezwa na kupewa sifa kemkem kwa mambo wanayoyafanya, hata kama ni madogo. Ukiwa na tabia ya kusifia na kumpongeza mwenza wako, basi utakuwa katika hatua nzuri ya kulihuisha penzi lenu lililofifia. Msifie kwa mapishi yake, msifie kwa urembo wake, msifie mkiwa kitandani na kwa mambo yote mazuri anayoyafanya. Ukifanya hivi, basi utakuwa na uhakika wa kurudisha penzi lililopotea.
Tembeleeni sehemu za burudani pamoja.
Kutembelea sehemu za starehe na sehemu za kitalii ni mbinu moja bora sana katika kurudisha penzi lililopoteza uhai wake. Panga safari fupi na mwenza wako na umpeleke maeneo ambayo yatamfanya ajisikie furaha na awe na raha wakati wote. Usijali kuhusu namna ya kuandaa safari hiyo kwani siku hizi kuna mawakala wengi wanaoshughulika na kuandaa safari kwa gharama nafuu kabisa.
Onesha kuwa unamjali.
Wapenzi wengi huhitaji wenza wao kuwajali kwa kila jambo. Unapokuwa humjali mpenzi wako basi una hatari kubwa sana ya kumpoteza. Jitahidi kuzikumbuka siku mbalimbali zenye kumbukumbu muhimu kama vile, siku yake ya kuzaliwa, penda kuhudhuria sherehe mbalimbali ukiwa nae na mambo mengine kama hayo. hapo utakuwa na uhakika wa kulihuisha tena penzi lenu lililokuwa limedhoofika.
Mnunulie zawadi mbalimbali.
Zawadi ni zawadi bwana. Hata kama ni ndogo, humfanya mwenza wako ajisikie furaha na kuhisi anapendwa. Jitahidi kumnunulia mwenza wako zawadi mara kwa mara na vitu vingine anavyovipendelea. Chunga tu visije vikawa nje ya uwezo wako.
Haya ni baadhi ya mambo machache tu ambayo unaweza ukayafanya ili kulihuisha penzi lenu lililodhohofika. Zipo namna nyingi, na wewe pia unaweza kuongeza mbinu nyingine unazoona kuwa zinaweza kurejesha penzi lililopotea kwa kuandika maoni yako hapa chini.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link