NEW UPDATES

MSANII WA FILAMU, IRENE UWOYA ATEULIWA KUWA BALOZI..soma zaidi...

2 hrs ago  Entertaiment

Kampuni ya simu ya Mkononi ya itel imemtambulisha Msanii Bongo Movie, Irene Uwoya kuwa Balozi wa kampuni hiyo hapa nchini.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Irene amesema amejisikia faraja kuwa balozi na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu.

Amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na kuweza kufanya makubaliano ya kuwa balozi katika kuunganisha itel na watanzania kwa ujumla.

Kwa upande Mkurugenzi wa itel, Coopeer Chan amesema kuwa wanatarajia jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa za kampuni hiyo kupitia kwa balozi Irene Uwoya katika matukio ya kuonyesha ukarimu kwa baadhi ya makundi kwa utoaji wa misaada.

Amesema kuwa wanamkaribisha balozi mpya itel Tanzania Irene Uwoya kuungana na familia ya kubwa ya itel.

“Sote tunafahamu mchango wa Irene Uwoya kwenye jamii amekuwa akielimisha kupitia filamu zake na kutambua umuhimu wake sisi itel Mobile tutashirikiana naye kikamilifu kuhakikisha jamii inapata kile inachotarajia kukipata kwetu na kwake pia” amesema Chan.

Mkurugenzi wa itel, Coopeer Chan akisaini makubaliano na Msanii Bongo Movis, Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency jijini Dar es Salaam.

Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akizungumza na waandishi wa habari juu kuwa balozi wa Kampuni ya Simu ya Mkononi leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Masoko wa itel, Asha Mzimbili akizungumza na waandshi habari juu makubaliano katika balozi mpya itel, Irene Uwoya leo jijini Dar es Salaam.

Mkuruegenzi wa itel , Coopeer Chan akibadilishana hati ya makubaliano na Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency jijini Dar es Salaam.

Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akiwa katika picha ya pamoja wafanyakazi itel leo jijini Dar es Salaam

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link