NEW UPDATES

WANASAYANSI ZIMBABWE, WAMEFAURU KUZALISHA MTOTO KWA NJIA YA " VITRO FERTILIZATION "

Kwa mara ya kwanza nchini Zimbabwe, wanasayansi wamefaulu kuzalisha mtoto kwa njia ya ‘vitro fertilization’ ambayo inahusisha kuunganisha mbegu za kiume na kike kwenye maabara na kisha kukuza mbegu hizo maabarani (nje ya tumbo ya mama) hadi mtoto anapoumbika.

Mtoto huyo alizaliwa baada ya wiki 29 akiwa na uzani wa kilo moja, mamake ambaye hakutaka kutambuliwa alisema. Licha ya kuzaliwa mapema na kuwekwa kwenye mitambo ya kumsaidia kupumua, mtoto huyo hakuonyesha dalili ya kuwa na matatizo ya kupumua. Mwanamke huyo ambaye amekuwa akijaribu kutafuta mtoto kwa miaka mitano bila mafanikio tangu kuolewa anatarajia kurudi na mtoto wake nyumbani wiki hii.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link