KIWANGO STAHIKI CHA CALORIES KWA MWANAMKE NA MWANAUME MWILINI
Direna health support
NINI MAANA YA CALORIE?
Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (°C).
Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi.
Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.
UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI.
Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai.
Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito.
Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.
MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI?
Kwa kawaida, mwanaume anahitaji Calorie 2500 ili aishi, na mwanamke anahitaji Calorie 2000 ili aishi. Maana yake ni kwamba, kama mwanaume atazidisha calorie Zaidi ya 2500 kwa siku, basi ataongezeka uzito, na pungufu ya hapo anapungua.
Kiwango hiki hutegemeana pia na shughuli ambazo mtu husika anazifanya. Kwa mfano mtu anayefanya mazoezi sana au kufanya kazi ngumu, atahitaji calorie nyingi Zaidi kuliko mtu ambae anafanya shughuli za kawaida.
JE, WINGI (UJAZO) WA CHAKULA HUMAANISHA CALORIE NYINGI?
Hapana, kila chakula, tunda, kinywaji au mboga mboga zina kiwango chake.
Tazama mfano huu…
Unaweza ukala bakuli zima kubwa la mboga za majani hadi ukashiba, na ukawa umekula calorie 400 tu.
Unaweza kula kipande kimoja cha kuku wa kukaanga, ukawa umeingiza calorie 400.
Na pia, unaweza ukatumia vijiko viwili vya mafuta ukawa umeingiza calorie 400.
Hivyo katika mifano hii, utagundua ya kwamba, ukila mboga mboga kwa wingi, utafanya tumbo lijae na kujihisi shibe, lakini ukawa umeingiza calorie kidogo, kuliko kusema ule kuku wa kukaanga hadi ushibe, itakufanya uingize calorie nyingi sana mwili kuliko mahitaji ya mwili.
Hivyo utaona ya kwamba, kwenye kupakua chakula, wanga unatakiwa uwe kiasi kidogo, lakini mboga mboga na matunda ndio viwe kwa kiwango kikubwa. (tofauti na ambavyo tumezoea ya kwamba chakula ndio kinakua kingi na mboga kua kidogo)
Imeandaliwa na:
BALDWIN KINUNDA
KAM COLLEGE FITNESS GYM
O627866044(whatsapp)
0746751879
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link