NEW UPDATES

WAJUE WANAWAKE WATONO WENYE USHAWISHI MKUBWA KATIKA HISTORIA YA AFRIKA


Katika historia y Afrika na kote duniani, wanaume peke yake ndiyo wamekuwa wakizungumziwa zaidi na kusahau kazi waliyoifanya baadhi ya wanawake.

Kwa jamii nyingi duniani, hasa za kiafrika, wanawake wamekuwa hawapewi kipaumbele kama walivyo wanaume. Ni hivi karibuni tu jitihada za kuwapa kipaumbele wanawake zimeanza kushika hatamu, baada ya kuibuka kwa makundi yanayotetea haki zao.

Tukiangazaia katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika kutoka kwa wakoloni, majina ambayo yatakuja katika akili yako ni pamoja na Nelson Mandela, Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba na wengine wengi.

ni vigumu sana kwa mtu kuanza kufikiri kuhusu wanawake waliochochea harakati za ukombozi wa bara la Afrika. Pengine leo ndiyo umetambua kwamba kuna wanawake waliochangia katika harakati za ukombozi.

Ndiyo, wapo wanawake ambao walikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi na kupitia wao baadhi ya mataifa ya Afrika yamepata ukombozi. Lakini cha kushangaza, wanaume ndio waliopewa sifa zote na wanawake hao kusahaulika.

Wafuatao ni wanawake ambao wamekuwa na nguvu ya ushawishi barani Afrika;

Yaa Asantewaa – Mkuu wa Majeshi

Hakuna mwanamke aliyejulikana katika historia ya kuupinga ukoloni barani Afrika kama Nana Yaa Asantewa wa himaya ya Asante Edweso huko Ghana. Alikuwa kiongozi wa majeshi kwa kile kilichojulikana kama ‘Vita ya Yaa Asantewa’ ambayo ndiyo vita ya mwisho kupiganwa baina na himaya ya Asante na Waingereza. Baadae Waingereza walimtambua kama Joan D’Arc wa Afrika’. Japokuwa hakuwa akienda vitani, ila majeshi yalipigana kwa amri na maelekezo yake, hata silaha za kivita kama unga wa risasi yeye ndio aliwapatia.

Funmilayo Ransome Kuti – Mwanaharakati

Kuti alikuwa moja ya watu muhimu katika mapambano dhidi ya ukoloni wa Waingereza nchini Nigeria. Ndiye mwanzilishi wa Umoja wa Wanawake wa Abeokuta ambao ulikuwa na lengo la kupinga kodi ya wakoloni. Kama mwanaharakati, Kui alipigania pasipo kuchoka haki za wanawake na uwakilishi wao katika siasa pamoja na kuyawezesha makundi ya chini ya jamii

Malkia Nzinga 

Anajulikana pia kama Malkia Jinga. Likuwa na tabia ya kuwaajiri wanawake katika nafasi kubwa za kiserikali katika nchi ambayo kwa sasa inajulikana kama Angola. Dada zake wawili walikuwa viongozi wa kivita na baraza lake la washauri liliundwa na wanawake wengi zaidi. Nzinga aliunda jeshi kubwa ambalo lilikuwa likiwapiga na kuwateka maadui wake, vilevile aliungana na majeshi mengine kuhakikisha kuwa wanamiliki njia za kibiashara ikiwemo ile ya watumwa. Amewahi kuungana na Waholanzi ili aweze kuwapiga na kuwashinda wakoloni wa Kireno. Baada ya jitihada za muda mrefu, alifanya mazungumzo ya amani na Wareno lakini bado alikataa kulipa kodi kwa wakoloni hao.

Ruth Williams, Lady Khama

Lady Khama  alikuwa mke wa Rais wa kwanza wa Botswana, Seretse Khama. Alizaliwa huko Blackheath kusini-mashariki mwa London na alikuwa mtoto wa Afisa mstaafu wa Jeshi la India. Yeye kuolewa na mwanaume mweusi ambaye alikuja kuwa Rais wa Botswana ilikuwa aibu kubwa kwa serikali ya waingereza ila iliwapa motisha wanaharakati waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi (Apartheid) nchini Afrika Kusini. Lady Khama alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi katika siasa wakati wa utawala wa mume wake. Mnamo mwaka 1980 mumewe, Seretse Khama alipofariki watu wengi walidhani angerudi kwao London, lakini badala yake alibaki Afrika na baadae alikuwa Rais wa chama cha msalaba mwekundu katika nchi yake ya Botswana.

Miriam Makeba – Mama wa Afrika

Huyu alikuwa mpinzani wa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini. Miriam Makeba alijulikana pia kama Mama Afrika. Makeba hakushiriki tu katika shughuli kubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi lakini pia katika harakati za kutetea haki za kiraia.


Share :

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link