NEW UPDATES

Orodha kamili ya mawaziri na manaibu wapya walio teuliwa na raisi magufuli.

ORODHA KAMILI YA MAWAZIRI NA MANAIBU WAPYA WALIOTEULIWA NA RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, ambapo baadhi ya mawaziri wamepoteza nyadhifa zao, wengine wakipandishwa nafasi na wengine wapya kuongezwa.

Rais amefanya mabadiliko pia katika wizara mbili ambapo wizara hizo zimegawanywa, jambo lililofanya wizara kuongezeka kufikia 21 kutoka 19 zilizokuwapo.

Wizara zilizogawnywa ni Wizara ya Nishati na Madini ambayo imekuwa wizara mbili zinazojitegemea, Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini pamoja na Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo imegawanywa kuwa Wizara ya Kilimo, na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mbali na mawaziri na manaibu wao, Rais Dkt Magufuli ametangaza kuteua Katibu Mkuu mpya wa Bunge.

Hapa chini ni orodha ya Mawaziri, Manaibu Waziri wapya walioteuliwa. Baadhi yao ni wapya katika baraza, huku wengine wakipandishwa kutoka manaibu kuwa mawaziri, na wachache wakihamishwa wizara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora- George Huruma Mkuchika (Mpya)Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)- Selemani Said Jafo (Amepandishwa kuwa Waziri)Naibu Waziri wa Wizara Muungano na Mazingira- Kangi Alphaxard Lugola (Mpya)Naibu Waziri wa Walemavu (Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) – Stella Ikupa (Mpya)Waziri wa Kilimo – John Tizeba (Alikuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi)Naibu Waziri wa Kilimo- Mary Chuki Mwanjelwa (Mpya)Waziri wa Mifugo na Uvuvi- Luhaga Mpina (Alikuwa Naibu Waziri Mazingira na Muungano)Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi- Abdallah Ulega (Mpya)Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano- Elias John Kwandikwa (Mpya)Waziri wa Nishati- Merdadi Kalemani (Alikuwa Naibu Waziri Nishati na Madini)Naibu Waziri wa Nishati-  Subira Khamis Mgalu (Mpya)Waziri wa Maliasili na Utalii- Khamis Kigwangalla (Alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya)Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii- Japhet Ngailonga Hasunga (Mpya)Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji- Mhandisi Stella Manyanya (Alikuwa Naibu Waziri Elimu)Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia akitokea Wizara ya Mifugo- William Ole Nasha (Alikuwa Naibu Waziri Kilimo Mifugo na Uvuvi)Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Juliana Daniel Shonza (Mpya)Katibu wa Bunge -Stephen Kagaigai. Aliyekuwepo, Dkt. Thomas Kashi Kashililah atapangiwa kazi nyingine.Waziri wa Maji na Umwagiliaji-Mhandisi Isack KamwelweNaibu Waziri Maji na Umwagiliaji – Jumaa Hamidu Aweso

Aidha, Rais Magufuli ametangaza kuwa, wale wote walioteuliwa ambao wataridhia uteuzi huo, wataapishwa Jumatatu Oktoba 9 saa 3 asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Share :

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link