NEW UPDATES

TCRA YAZIBANA KAMPUNI ZA SIMU NCHINI

TCRA YAZIBANA KAMPUNI ZA SIMU NCHINI

hour ago  Kitaifa

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka kampuni za simu za mikononi kusitisha matangazo wakati wateja wanapiga simu vinginevyo wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kulaba amesema kuwa, wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wateja mbalimbali wakisema wanawekewa matangazo na kampuni ya simu mara wanapopiga simu badala ya kuunganishwa moja kwa moja na wanaowapigia.

“Kuna matangazo yanayowataka wateja kujiunga na huduma za miito zinazosikika kabla ya kumuunganisha mpiga simu na yule anayempigia. Pia yapo yale matangazo yanayotokea wakati unapompigia mtu simu halafu akawa anaongea na simu nyingine au hapatikani kwa wakati huo. Kumpa mtu matangazo bila ridhaa yake kabla ya kumpa huduma anayoitaka mpigaji hivyo kumpotezea muda wake,” alisema Kulaba.

Aidha, Kubala alieleza kwamba, kanuni za kulinda mtumiaji wa huduma za mwaka 2011 zinataka watoa huduma kuweka matangazo yao wakatika wakituma ujumbe kwa mteja anapouliza/kuangalia salio la muda wa maongezi.

Alisema pia kanuni hizo zinamtaka mtoaji huduma atoe huduma husika kwa muda muafaka na kwa kutumia lugha inayoeleweka.

Kulaba amezionya kampuni za simu ambazo zinafahamu kuwa sheria ipo lakini zimekuwa zikikiuka kwamba, kuanzia leo zikirudia zitakumbana na sheria.

Akitaja baadhi ya adhabu zinazoweza kutolewa kwa kampuni itakayokiuka sheria, Kulaba alisema ni pamoja na faini au kufungiwa kufanya kazi nchini.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link