NEW UPDATES

PCCB

Viongozi wawlili wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam, Diwani wa Kata ya Msigani, Israel Mushi (48) na Mrasimu Ramani wa Manispaa, Francis Mwanjela (28) wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kuomba na kupokea ya shilingi milioni 5.

Mkuu wa TAKUKURU Kinondoni, Teddy Mnjagira alisema katika taarifa yake kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Jumatano baada ya kupokea kiasi hicho cha pesa kutoka kwa mwananchi ambaye mbali na kutoa pesa hiyo alitakiwa na watuhumiwa kuwapa rushwa ya shilingi milioni 10.

“Tumewakamata watu wawili ambapo mmoja ni Diwani na mwingine ni Mrasimu wa Ramani wa Manispaa ya Ubungo ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kuomba, kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi milioni tano,” alisema Mnjagira.

Watuhumiwa wanadaiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango ya miji inayoshughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo.

Uchunguzi watuhuma dhidi yao unaendelea na watuhumiwa hao wanaohusishwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 wamepewa dhamana.

Mnjagira amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kuwafichua wanaojihusisha na vitendo vya rushwa ili wachukuliwe hatua za kisheria.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link