MBINU ZA BIASHARA NILIZO JIFUNZA MWAKA 2017
Baadhi ya mambo muhimu sana kuhusu majadiliano ya kibiashara nilijifunza kutoka kwa babu yangu ambaye alihusika tafiti na maendeleo ya viwanda vyote vya kampuni mbali mbali. Siku za Jumamosi alikuwa akinichukua na kunipeleka gereji ili niongeze ujuzi.
Ingawa kumekuwa na mabadiliko makubwa sana ya teknolojia toka kipindi hicho alipokuwa hai, mafunzo ya msingi katika kujadiliana na kufikia muafaka na watu yamebaki kuwa yaleyale. Jifunze kuepuka sana makosa ya mara kwa mara ya kukosea kwenye kauli zako unazozungumza wakati wa majadiliano, kama mafunzo haya niliyoyapata utotoni mwangu:
1. Usijikandamize wewe mwenyewe
Kanuni ya kwanza ya majadiliano ni: Usijiumize wewe mwenyewe.
Nilipokuwa mdogo, nilinunua kompyuta kwa kupiga simu tu baada ya kuona tangazo lilioandikwa “punguzo kubwa la bei,” wakati huo babu yangu alikuwa akisikiliza nilipokuwa nafanya mazungumzo na muuzaji. Baadaye akaniambia, “Umeongea vizuri sana ulipokuwa unazungumzia bei. Na kuna kitu inabidi ukizingatie mara nyingine ukiwa unanunua kitu — usijikandamize wewe mwenyewe katika mapatano ya bei.”
Alipoona namshangaa baada ya kuniambia hivyo, akasema: “Tangazo uliloliona liliandikwa ‘punguzo kubwa la bei.’ Lakini tangazo halikukwambia bei yenyewe ni kiasi gani. Kwahiyo unajikuta wakati unazungumzia bei ya kununua kitu, huna hata fununu kama wanataka kukuuzia kwa shilingi elfu moja, laki moja au milioni moja. Wewe umemwambia utalipa shilingi laki tano bila hata kujua hiyo kompyuta ilikuwa inauzwa shilingi ngapi mwanzo na baada ya punguzo imekuwa shilingi ngapi. Kwahiyo umejiumiza wewe mwenyewe kwenye maongezi yenu.”
Usiwe wa kwanza kutaja bei ya kununua unachokitaka, muache muuzaji wa kitu unachotaka kununua ataje bei yake kwanza kisha mjadiliane punguzo kutokea hapo.
2. Usiwe na tabia ya kuomba omba sana
Kanuni ya pili kwenye majadiliano ya pesa ni: Usiwe na tabia ya kuomba kiasi kikubwa sana. Mara zote taja kiasi ambacho hakiwezi kumuumiza mtu mwingine.
Babu alikuwa akiniambia, “Nguruwe huwa wanalishwa, lakini wakinenepa sana wanachinjwa.” Kwa muda mrefu sana sikuelewa maana ya kauli hii lakini baada ya miaka kupita sasa najua inamaanisha — omba kiasi kinachoweza kukutatulia shida yako tu, usizidishe.
Ukiwa unaomba kiasi kikubwa sana cha pesa, utaua mpango mzima, iwe unataka kununua kompyuta, kuomba uongezewe mshahara au mkataba wa kazi, kama ukiwa una maombi makubwa sana, utaua mpango huo na hutafikiriwa kabisa inapotokea nafasi yoyote siku zinazofuata.
Mafanikio kwenye biashara yanategemea sana uwezo wako wa kujenga mahusiano ya muda mrefu na watu wengine na sio kwa kuhakikisha unachukua kila senti iliyomo mfukoni mwa mteja wako.
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link