KESI YA DAWA ZA KULEVYA YA YUSUF MANJI YAENDELEA TENA
Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabishara maarufu nchini, Yusuf Manji imeahirishwa hadi Agosti 10 mwaka huu baada ya upande wa jamhuri kusema kuwa upelelezi haijakamilika.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu, Cyprian Mkeha aliahirisha kesi hiyo Julai 6 baada ya wakili wa serikali kusema mahakamani hapo kuwa upelelezi haujawa tayari.
Manji ambaye ni Diwani wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, hakuwepo mahakamani hapo wakati kesi hiyo ikiendelea.
Katika kesi ya msingi, Yusuf Manji anatuhumiwa kati ya Februari 6 na 9 mwaka huu katika eneo la Upanga Sea View, Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo Februari 16 mwaka huu, Manji alikana na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Tsh 10 milioni
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link