NEW UPDATES

VIFAHAMU AINA YA VYAJULA VITAKAVYO KUSAIDIA KUEPUKA KITAMBI

VIFAHAMU AINA YA VYAKULA VITAKAVYOKUSAIDIA KUEPUKA KITAMBI

5 days ago  AfyaMakala

Watu wengi hupata wakati mgumu sana kupunguza miili yao baada ya kunenepa na wengine kuishia kujichukia kotokana na wao kuwa na maumbo ambayo hawayapendi.

Hali hii hutokea zaidi kwa wanawake ambao mara nyingi huwa ni wavivu au wanakosa motisha ya kufanya mazoezi ambayo yatawasaidia kupunguza miili yao. Kabla haujanenepa, ni muhimu kujua ni chakula cha aina gani unakula na kwa kiasi gani ili kuepuka kunenepa vitambi ambavyo vitakufanya usiwe na furaha.

Lakini unene/vitambi si tu vinakufanya uwe na umbo lisilovutia, bali pia huweza kukusababishia magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo. Hapa chini ni orodha ya vyakula vitakavyokusaidia kuepukana na kitambi hasa kwa wanawake.

Siagi ya karanga

Siagi ya karanga kazi kubwa inayofanya ni kukusaidia wewe kutokusikia njaa kila mara na pia huongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Kama siagi itakufanya usisikie njaa, inamaana itakusaidia kujizuia usile vyakula ambavyo vingeweza kukuletea wewe kitambi.

Lakini pia, siagi ya karanga ina kiinilishe kijulikanacho kama niacin ambacho huzuia mafuta kujilundika mwilini (tumboni). Unapokuwa unakula mkate, unashauri kutumia siagi ya karanga.

Mayai

Mayai ya kienyeji yana vitamini nyingi ndani yake na madini kama vile kalshiamu, zinki, chuma na omega. Viinilishe vyote hivyo katika mayai husaidia kuchoma mafuta yanayozidi tumboni. Hivyo, unashauriwa kula mayai kila siku asubuhi ili kupunguza mafuta mwilini.

Mbali na hilo, mayai pia yanaweza kukufanya ujisikie kushiba kwa muda mrefu na kuwa huhitaji kula chakula kingine.

Chai ya kijani (Green Tea)

Chai ya kijani husaidia kuondoa sumu mwilini jambo linalosaidia picha kuchoma mafuta ndani ya mwili wako. Kunywa chai hii mara kwa mara kutakusaidi kupunguza sumu mwili mwako na pia tumbo lako kuwa sawa.

Aidha, unashauriwa kuwa usiweke sukari katika chai hii wakati unapokunywa.

Mtindi

Ingawa mtindi unaweza kukusababishia ongezeko la uzito, ukinywa bila kuongezwa kitu ndani yake, utakusaidia kupunguza mafuta tumboni. Matumizi yake kwa siku hayatakiwi kuzidi kikombe kimoja (glasi moja).

Pia mtindi utakufanya ujisikie umeshiba na hivyo kukuondolea hamu ya kula mara kwa mara jambo linazoweza kukusababishia uzito na kuongeza mafuta.

Ndizi mbivu

Ndizi mbivu ni muhimu kwa afya yako kwani zina wingi wa madini ndani yake kama vile potasiamu na vitamini za aina mbalimbali. Ndizi hukuondolea hamu ya kula kila wakati.

Vile vile ndizi huupa mfumo wa mmeng’enyo cha kula nguvu hivyo kusaidia kuyeyusha mafuta yaliyopo tumboni kwa urahisi zaidi.

Maji

Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito. Kunywa maji lita tatu kila siku kutasaidia kuondoa sumu mwili mwako lakini pia itasaidia ngozi yako kuwa salama. Jiwekee utaratibu kuwa kila unapoamka asubuhi hata kabla ya kuswaki, kunywa maji angalau glasi mbili.

Baada ya kuanza kazi zako za siku, kunywa maji angalu glasi moja kila baad ya saa moja.

Kuhusu upande wa chakula, hapo tumeelezea tu kwa uchache lakini bado kuna vingine vingi kama nyama, samaki, mboga za majini, maharage.

Pia epuka sana kula vyakula vyenye sukari na pia wanga kwani chakula unachokula ni nishati kwenye mwili wako, hivyo ukiweka nishati nyingi halafu usipoitumia, mwili utaiifadhi kwa ajili ya matumizi ya siku nyingine. Kumbuka, weka nishati unayoihitaji tu. Pia epuka kula chakula muda mfupi kabla ya kulala.

Mbali na vyakula tulivyovitaja hapo tu, jambo jingine kubwa la kuzungati ni kufanya mazoezi kila mara. Jitahidi kufanya mazoezi angalau mara nne kwa wiki na kila siku utumie si chini ya dakika 30. Unaweza kukimbia, kutembea umbali mrefu, kuruka kamba.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link