NEW UPDATES

EPUKA KUMFANYIA MAMBO HAYA MCHUMBA WAKO.

Makala

Kipindi cha uchumba kinachokuliwa kuwa kipindi muhimu sana kwa wachumba kufahamiana na kujuana; kujua wanachokipenda na wasichokipenda, kujua sifa na silika zao pamoja na mambo mengine mengi.

Wahusika wanaweza wakapitia nyakati ngumu kwa sababu ya uelewa mbaya na kuyapuuza mambo mambo madogo ambayo hugeuka kuwa kizingiti kwenye uhusiano wao. Hivyo, dada yangu jiepushe na mambo ambayo husababisha migogoro na kukuingiza kwenye mzozo ambao sio wa lazima kwako pamoja na mumeo mtarajiwa. Hapa ninakuletea mambo ambayo unatakiwa kuepuka kumfanyia mchumba wako:

1.    KUTOMUAMINI:

Usirudierudie kumuuliza kuhusu anachowaza hasa mnapokutwa na tatizo, ni upi uamuzi wake na atafanya nini; kwa sababu maswali mengi ni dalili ya kutomuamini.

2.    KUIBUA WIVU:

Wivu ni mzuri, usipovuka mipaka. Ukivuka mipaka kwa kuzusha wivu na mchumba wako mambo yatakugeukia na hutaweza tena kuyaweka sawa.

3.    KUMLINGANISHA NA WENGINE:

Usimlinganishe na yeyote. Baadhi ya maneno yanaweza kumbebesha mzigo ambao hatoweza kuubeba na hivyo kuwa na radiamali hasi dhidi yako kwa kuona kuwa ameshindwa kukuridhisha.

4.    USIOGOPE TOFAUTI ZENU:

Iwapo kuna mambo mnayorandana basi mwambie. Kwa mfano, kupenda kusoma au kufanya mazoezi maalum. Iwapo hayapo, basi usiogope kwa sababu sio udhaifu huo. Uwepo wa tofauti kati yenu ni jambo zuri kwa kuwa litawafanya mkamilishane na hivyo kila mmoja kuwa mhitaji wa mwenzie.

5.    KUMCHUNGA:

Usiwe mtu wa kuuliza muda wote: “Kwa nini hukunipigia? Kwa nini hukupokea simu yangu? Ulikuwa wapi? Ulikuwa na nani?” usifamye ahisi kuwa unamchunga  na kumfuatilia, mpe fursa ya kuwa na uhuru.

6.    UKOSOAJI KAYAYA:

Epuka sana kumkosoa mkiwa pamoja au hata mbele ya ndugu zenu; kwa sababu siku ya kwanza anaweza akaliweka moyoni au akaliacha likapita, lakini ukirudiarudia hilo hatolivumilia au litaibua hasira yake na kukufanya ujute.

Dada yangu, jiepushe sana na mambo hayo ambayo yanaweza kuibua matatizo ambayo mara nyingi hupelekea watu wakaachana. Unatakiwa kuwa muwazi lakini usivuke mipaka au kuwakera wengine ili uweze kufurahia maisha matamu ya ndoa yaliyojaa maelewana na upendo hapo baadaye.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link