NEW UPDATES

ASHINDA BILIONI 4 KWA KUBASHIRI (BETI) MATOKEO YA MPIRA WA MIGUU

ASHINDA BILIONI 4 KWA KUBASHIRI (BET) MATOKEO YA MPIRA WA MIGUU

KENYA: Samuel Abisai, amepata bahati ya kujishindia kitita cha jumla ya shilingi za Kenya milioni 221 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 4.8 katika mchezo wa kubashiri kupitia kampuni ya SportPesa.

Mshindi huyo aliyetangazwa siku ya Jumanne katika ukumbi wa ‘Carnivore Restaurant’ ulioko jijini Nairobi alishinda baada ya kubashiri kwa usahihi michezo 17.

Kitita hicho alichokishinda Samwel, kinaweza kutumika kumlipa mchezaji wa Tottenham Hotspur raia wa Kenya, Victor Wanyama kwa muda wa miezi 7 na siku 11.

Siku ya Jumatatu, SportPesa walisema kuwa mshindi huyo aliweka Ksh 200 (TZS 4,338) katika ‘mega jackpots’ mbili akitumia Ksh. 100 kwa kila moja, na walipompigia simu, Samwel alikuwa ametambua kuwa ameshinda tayari na alishaanza kushangilia.

“Samwel alikuwa na wenzake aliobashiri nao wakijadiliana kitu cha watakachofanya na fedha hizo wakati alipopigiwa simu na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Ronald Karauri” walisema SportPesa.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link