SABABU ZINAZO SABABISHA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA
Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakipatwa na maumivu makali kila wanaposhiriki tendo la ndoa (kujamiana).
Kutokana na tatizo hilo kuna baadhi ya wanawake wamejikuta wakilichukia tendo hilo na yao hata kuhatarisha ndoa zao.
Leo nimeona niweze kukueleza msomaji wangu hasa wewe mwanamama mwenye tatizo hili kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia hali hiyo ya maumivu ni pamoja na hizi zifuatazo hapa chini:-
1. Ukosefu wa ute ute sehemu za siri ambao husaidia kupunguza msuguano wakati wa tendo hilo. Mara nyingi uteute huo hutokana na maandalizi ya kutosha ambayo huweza kufanyiwa mwanamke na mwenzi wake.
2. Maambukizi, mfano fangasi, U.T.I pamoja na magonjwa mengine ya zinaa huweza kupelekea hali hiyo pia ya kuhisi maumivu wakati wa tendo. Hivyo unapoona hali hiyo ni vyema kufika hospitali iliyokaribu nawe ili uweze kufanyiwa uchunguzi zaidi.
3. Pia kuhisi maumivu hayo huweza kuashiria uwepo wa vijiuvimbe vidogovidogo kwenye njia ya uzazi 'fibroid' hivyo ni vyema kuwaona wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi unapohisi hali hiyo.
4. Kwa wale ambao huenda hutumia kinga (kondom) nao huweza kupatwa na tatizo hili la maumivu wakati wa tendo, hivyo unapohisi hali hiyo unaweza kubadilisha aina ya kondomu kwani baadhi ya kondomu zinaweza kutowafaha aina fulani ya watu kwa sababu mbalimbali zikiwemo za mzio 'allergy'.
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link