NEW UPDATES

ROMA MKATOLIKI NA WEZAKE KUPATIKANA.

Msanii Roma Mkatoliki na wenzake watatu wamepatikana leo waki hai baada ya kutoweka kwa kutekwa siku ya Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records.

Roma Mkatoliki na Moni Cetrozone


Baada ya taarifa ya Kamishna wa Polisi Kamanda Simon Sirro iliyotolewa leo asubuhi na kusema polisi wanaendelea na upelelezi, wasanii hao wote wamepatikana wakiwa hai na sasa wapo katika kituo cha polisi cha Oysterbay.

Mmiliki wa wa Tongwe Records J Murder amethibitisha wasanii wake hao kupatikana na sasa wapo kituo cha polisi wakitoa maelezo.

Mpaka wakati huu mke wa Roma Mkatoliki amefika kituoni hapa hapa na kuambiwa wasubiri nje utaratibu wa kipolisi uendelee kufanyika. 

Tutaendelea kukujuza kinachoendelea kuwa nasi. 

 

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link