MABILIONEA WAWILI WA TANZANIA WANUNUA KAMPUNI KUBWA YA MAFUTA AFRIKA
Habari kitaifa
Mabilionea wawili raia wa Tanzania Aunali na Sajjad Rajabali wamenunua hisa milioni 30.2 sawa na asilimia 2.06 ya hisa zote katika kampuni ya mafuta ya KenolKobil.
KenolKobil ni kampuni kubwa ya mafuta barani Afrika ambayo inajishughulisha na uuzaji wa bidhaa hiyo katika nchi saba zilizomo Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1959.
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka iliyotolewa na kampuni hiyo, hisa hizo zina thamani ya shilingi 8.2 bilioni katika soko na kuwafanya Rajabali kuwa nafasi ya 9 kati ya wawekezaji 10 bora wa kampuni ya KenolKobil.
Ndugu hao wawili mabilionea wamewekeza jumla ya TZS 15.1 bilioni katika kampuni mbili za Benki ya Ushirika na Kenol.
Wawili hao wanafanya kazi kwa ukaribu na Benki ya CRDB nchini Tanzania na uamuzi wao wa kununua makampuni hayo mawili makubwa unaonyesha wanaimani na mafanikio ya kampuni hizo katika miaka ijayo.
Kampuni ya Kenol ilipata faida ya TZS 52 bilioni kwa mwaka jana ikiwa imechangiwa na mauzo makubwa, katika nchi inazofanya kazi pamoja na gharama ndogo za uendeshaji.
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link