Kamanda sirro kumaliza utata kuhusu Roma
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ameahidi kuzungumzia suala la kutoonekana kwa wasaanii Roma Mkatoliki na Moni wa Centrozone tangu usiku wa kuamkia jana Alhamisi walipochukuliwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kwa kusipojulikana.
Akitoa taarifa kwa wanahabari Katibu wa wa Chama cha Wasanii wa kizazi kipya TUMA, Bryton amesema baada ya kuhangaika kuwatafuta wasanii hao bila mafanikio Kamanda Sirro ameahidi kuzungumza na wanahabari na kutolea ufafanuzi ni wapi walipofikia kama chombo cha usalama.
Aidha Bryton ameongeza kuwa hakuna kiki ambazo zinatengenezwa kama jinsi baadhi ya watu wanavyoendelea kupotosha watu huku akiongeza kwamba tukio la kuchukuliwa kwa wasanii hao ni jambo la kutisha nalinazidi kuwatia hofu na halipendezi.
"Hili tukio siyo la kupendeza hata kidogo na linafanya wasanii waishi kwa mashaka. Hatuna amani kuanzia wasanii mpaka familia ya Roma. kilichotufanya leo tuwaite ni kuweka hili suala lieleweke na wala siyo kiki kama jinsi watu wanavyofikiri, jambo hili wanatakiwa walichukulie very serious siyo mzaha. Kamanda Sirro atalizungumzia kwa uzuri kesho saa tano kwa sababu bado wanaendelea kuwatafuta"Alizungumza Bryton.
Bryton - Katibu
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link