ZARI, WEMA UZAZI WA MPANGO. KITANZI, VIDONGE, VIJITI AU KONDOM ???
..
Uzazi wa mpango ni jambo muhimu sana kuzingatia katika jamii yetu, lakini kuna njia nyingi sana ukitaka kupanga uzazi, na familia nyingine walio Tumia uzazi wa mpango wanasema hawajutia kutumia njia hizo....
Lakini najiuliza ni njia gani iliyo sahihi na nzuri ya kutumia? Kwasababu watu wengine hupendelea kuweka vijiti Japo wengine husema vijiti hivyo hutembea mwilini na kuleta madhara ya cancer.
Wengine hutumia kitanzi, hiki hukaa muda mrefu wa miaka kumi, lakini pia wengine husema tatizo la kitanzi style yake kamwe ni kifo cha mende tu maana ukijifanya unatoa machejo kinafyatuka, na wengine wanasema mwenza wako akiingia kinamtia kero kwa kumgasi.
Nawengine wanatumia vidonge, lakini hata hivyo wengine husema ukikosea kumeza hata kimoja tu na ukacheza Basi goli lazima liwe lako, na wengine wamepata ujauzito pindi wanatumia hizi dawa. Ama kutumia kondomo?? Sawa mwanzoni mnaweza kutumia kondom lakini mpaka lini, maana wanaume wengi wanasema "yaani mke wangu mwenyewe nimvalie kondom???????????
Ama kwawale walevi najua pindi pombe zimekolea ni vigumu sana kukumbuka kondom.
Je wewe umeshawahi kutumia njia za uzazi na ni IPI? Maana kuna wanawake wanaohitaji kutumia njia hizi lakini hawajui ipi ni salama maana maneno yanasemwa mengi.
@Bakihotnews
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link