UTOKWAJI WA UCHAFU NI TATIZO LINALO KUMBA WANAWAKE WENGI WA MIJINI. Nikwasababu zifuatazo:-
Ikumbukwe kwamba
kutokwa na maji maji au ute katika via vya uzazi vya mwanamke ni jambo la kawaida wakati ambao mwanamke bado ana umri uzazi wa kuzaa, ikiwa ni sehemu ya mwili kuondoa sumu.
Ute huu kwa kawaida hauna rangi hadi ukikauka juu ya nguo na ndani ndiyo huashiria rangi nyeupe au njano.
Hata hivyo, hali hii huwa kwa kiasi kidogo ambacho hakihitaji mwanamke kuvaa kitu kingine zaidi ya nguo ya ndani ya kawaida ili kuzuia. Lakini maji maji hayo huashiria ugonjwa wa hatali yanapo kuwa yanaambatana na dalili zifuatazo:-
> Maji maji au ute kubadilika rangi na kuwa kama maziwa mtindi, chokleti, njano
kijani rangi ya usaha na au rangi ya juice ya parachichi.
> Maji maji yakiambatana na harufu mbaya hata kama mwanamke ameoga na kuvaa vizuri.
Kuna wakati harufu inakuwa kama shombo la samaki hasa wakati
wakushiriki tendo la ndoa na Baada.
> Ute una zidi kiwango çhake cha kawaida cha kila siku(abnormal quantity of discharge)
> Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa, pia maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
> Kuwasha sehemu za nje na ndani za via vya uzazi vya mwanamke.
> via vya uzazi kuwa na rangi nyekundu kuliko rangi yake ya ngozi ya siku zote.
> Muwasho sehemu za mlango wa via vya uzazi kwa ndani.
> Maumivu chini ya kiuno, Mbele na nyuma pia chini ya kitovu na hasa kushoto na kulia.
> Sehemu ya nje ya via vya uzazi kuwa vyekundu na wakati mwingine wekundu huo kuambatana na michubuko, vidonda na maumivu.
Sehemu ya nje (vulva) ya via vya uzazi kuwa nyukundu na wakati mwingine wekundu huo huambatana na michubuko, vidonda na maumivu.
SABABU YA UGONJWA AU CHANZO CHA TATIZO:-
Maambukizi au mashambulizi katika njia ya uzazi ya mwanamke na si njia ya mkojo hutokana na kufanya mapenzi yasiyo salama na mtu ambaye anamagonjwa ya zinaa, Hivyo bacteria, virusi au fangasi hushambulia njia ya uzazi.
Maambukizi hayo yapo ya aina kubwa tatu ambayo kitaalam ni:-
- Bacterial vaginosis,
- Trchoniasis na
- Monilia.
Kufanya mapenzi kinyume na maumbile na wakati huo huo kuhamia kwenye uke na kuamsha uchafu na wadudu ambao ushambuliwa njia ya uzazi.
Ulaji mbovu........
Utokwaji wa uchafu ni tatizo linalo kumba wanawake wengi wa mjini kwasababu ya ulaji mbovu wa vyakula.
Chakula chenye mafuta kinachochea au kuamsha seli za mafuta (fat cell) mwili mzima na hivyo kuzalishwa kwa homoni nyingi za estrogen.
Homoni hizi zikiambatana na upungufu wa fiber huchochea ukuaji wa bakteria wa ndani ya utumbo ambao kitaaramu wanaitwa CLOSTRIDIA
Hawa wana sifa ya kubadilisha bile acid kuwa homoni za estrogen ambazo zinapozidi sana husababisha tatizo la mwanamke kutokwa na uchafu katika via vyake vya uzazi.
Njia za kisasa za uzazi wa mpango (hasa vidonge) bila kujali ushauri wa kitaalam na bila kujari usafi husababisha kuaribika kwa ukutà wa uke kwani huufanya na hali ya alkali ambayo huruhusu au huchochea bakteria na fangasi kuvamia na kuzaliana, hasa candida albicans huzaliana sana na kushambulia uke.
Kutowiana kwa homoni za mwanamke.
Hali hii inasababisha na vyanzo vingi, mfano uzito kupita kiasi, ujauzito, wakati wahedhi, n.k
Uchafu wa mavazi na uchafu wa mwili hasa mwanamke ambaye hajui jinsi ya kujisafisha katika via vyake vya uzazi ili kuondoa seli zilizo kufa( deed cell)
SABABU YA UGONJWA AU CHANZO CHA TATIZO
Maambukizi au mashambulio katika njia ya uzazi ya mwanamke na sio njia ya mkojo hutokana na kufanya mapenzi yasiyo salama na mtu ambaye anamagonjwa ya zinaa,
Hivyo bakteria , virusi au fangasi hushambulia njia ya uzazi.
Maambukizi haya yapo ya aina kubwa tatu ambayo kitaalam ni bacterial vaginosis, Trchomoniasis na monilia
BAADA YA KUONA SABABU ZA KUTOKWA NA UCHAFU KWENYE VIA YA UZAZI, TUZUNGUMZE MADHARA YA KUTOKWA NA UCHAFU HUO ( Vaginal discharge)
UGUMBA:- Hii hutokea pale mashambulizi / maambukizi yanapofikia kwenye mirija na kuleta uvimbe ambao huziba au kusababisha kutengenezwa kwa maji machafu mzito ambayo nayo huziba mirija na huua mimba kila unapo tungwa.
MWANAMKE KUNUKA /KUTOA HARUFU :- Ambayo hutoka wakati wote hata kama ameoga na kuvaa vizuri.
Hali huwa mbaya zaidi wakati wa kushiriki tendo la ndoa, jambo hili husababisha mwanamke kuwa na aibu na kujitenga , kutengwa , kujiona hana thamani na unyonge.
KUPATA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO YAANI ( U.T.I)
.Hii ni kwasababu njia ya uzazi na ile ya mkojo zimekaribiana sana sehemu zinapo anzia kwenye via vya uzazi vya mwanamke.
Maumivu wakati wa kutoa haja ndogo, kwenda haja ndogo Mara kwa Mara na kutoa haja dogo yenye rangi ya njano au kijivu ni baadhi ya dalili za U.T.I.
Unashauliwa kumuona daktari Mara tu unapo jihisi au kuona mabadiliko tofauti katika mwili wako.
MWISHO:-
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete