NEW UPDATES

Mwongozo wa kuandaa harusi Tanzania

 


2 Comments
13768

Kwa wengi wetu, siku ya harusi ni siku tutakayokumbuka maishani. Na hivyo, inakuja na presha nyingi.

Zaidi ya hapo, harusi za kitanzania zina sherehe nyingi kabla ya siku ya kuoana, zikiwemo:

  • Mahari
  • Bridal Shower
  • Kicheni Pati
  • Begi Pati
  • Send-Off
  • Harusi (Kanisani na sherehe ya baada)

Ila, harusi zina tofautiana kutegemean na dini ya maharusi.

Aidha, kwa kawaida kamata zinaundwa na wanafamilia ya mahaurusi ili kuandaa sherehe hizi, hasa za siku ya harusi.

Iwapo unategemea kufanya harusi ya kitanzania zaidi au ya kisasa, mwongozo huu utakusaidia:

1. Unataka nini?

Kabla ya kumwajiri mtu wa kupanga harusi au kuunda kamata, jiulze ni nini haswa unachotaka kwenye harusi yako:

  • Kuna insha yoyote unayotaka?
  • Unataka ifanyike kwenye eneo fulani?
  • Unataka kuoa/kuolewa msimu gani?
  • Ungependa watu wa ngapi wawepo? Kwa kukadiria

Ukijibu maswali haya, unaweza kuendelea.

2. Bajeti

Watanzania wanautamaduni wa kuchangia harusi. Kwa hiyo, bajet yako itategemea kiasi cha michango yako.

Ila, siku za hivi karibuni maharusi (pamoja na wazazi wao) wanalipia harusi.

Chochote utakachoamua, fikiria:

  • Gharama za kukodi ukumbi
  • Gharama ya chakula
  • Gharama ya vinywaji
  • Usafiri
  • Wapiga picha na video
  • Mapambo
  • Gauni ya bibi harusi na vifaa vyake
  • Mavazi ya wapambe wa bibi harusi na bwana harusi (kama utakuwa unazilipia)
  • Maua ya harusi
  • Keki ya harusi
  • Burudani
  • Urembo
  • Pete za ndoa
  • Fungate
  • Zawadi za shukrani

Kumbuka, usitumie pesa yako yote kwenye harusi. Harusi ni muhimu, ndoa ni muhimu zaidi.

3. Ukumbi wa harusi

Kwa sherehe zote utakazofanya, kumbuka:

  • Hali ya hewa
  • Parking
  • Upatikanaji
  • Gharama

Kumbuka, send off na sherehe ya baada ya ndoa kufungwa ndio zenye watu wengi.

Tafuta ukumbi ya harusa hapa.

4. Mapambo

Inapendekezwa kuwa na rangi pekee za harusi zitakazo tumika kama mwongo wa mapambo na hata mavazi ya wageni. Kujua ni insha gani unayotaka kwenye harusi yako itakusaidia nah ii.

5. Kadi za mualiko

Kadi za mualiko inabidi ziwa za rangi ya harusi. Kama unashere nyingi za harusi, utahitaji kadi za mualiko mingi.

Unaweza ukairembesha kwa namna yoyote utakayopenda.

6. Muziki na Burudani

Watanazania wanapenda muziki na kucheza, hasa kwenye sherehe. Kwa hiyo, hakikisha kwamba atakaye wapigia muziki (awe kupitia DJ, bendi au wote wawili) ana ujuzi.

Bahati nzuri, kuna DJ na bendi nyingi wa kuchagua.

7. Chakula

Ukiwa unachagua kampuni ya mapishi, jaribu kuonja kila kitu watakachopika kwa ajili ya sherehe, kabla ya sherehe yenyewe.

Pia, hakikisha kuna chakula cha kutosha.

Pitia baadhi ya makampuni ya mapishi, hapa.

8. Vinywaji

Hakikisha kuna vinywaji vya kutosha vya aina mbalimbali, vyenye kilevi na visivyo na kilevi.

9. Usafiri

Kodi kampuni inayotoa huduma ya usafiri kwa ajili ya siku ya harusi.

Chagua kampuni bora inayotoa huduma ya usafari hapa.

10. Wahudumu

Kama ukumbi haitatoa wahudumu, kuna kampuni nyingi yenye huduma hii.Huduma ni muhimu sana kwenye sherehe kama hii kwa hiyo usibane matumizi hapa.

11. Nguo za harusi

Iwapo gauni la harusi ni vazi muhimu zaidi, itabidi uchague zingine kwa ajili ya sherehe zingine, wapamba wa harusi, wapambe wa bwana harusi na sherehe zingine za harusi.

Kumbuka swala la muhimu – ndoa

Kuna vitu vingi vya kupanga kabla ya harusi, na hivyo zinaweza zikakupa shida sana. Ila kumbuka, siku ya harusi ina umuhimu wake lakini ndoa ndio muhimu kuliko vyote.

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link