Njia za Kuingiza Pesa Kupitia YouTube Channel.
Bakihotnews
Wasanii au mtu yoyote mwenye channel iliyothibitishwa na Youtube anaweza kuingiza kipato kupitia matangazo yanayowekwa katika video mfano wa matangazo hayo ni matangazo ya video(Skippable Ads) ambayo huanza kuonekana kabla ya video husika kuanza kucheza
pia kuna matangazo ya graphics(overlay) ambayo hutokea ndani ya video huwa yanaonekana zaidi chini ya video na mengine huonekana nje ya video pembeni.
Matangazo haya huwa yanatolewa kupitia mfumo wa matangazo kwenye mitandao unaojulikana kama adsense ambao unamilikiwa na google na hela inayopatikana kupitia haya matangazo hugawanywa kwa asilimia kati ya Youtube na mtu anayemiliki channel ya Youtube inayodisplay matangazo hayo mfano msanii au mtu yoyote anayemiliki channel ya youtube na malipo hufanyika kupitia Western Union,Cheque au Wire Transfer kwenda kwenye account ya Bank.
Watu wengi wamekuwa wakitumia vibaya mfumo huu kwa kupakia video zinazohamasisha ngono,mauaji,ubaguzi au kuiba na kupakia video amabazo hawazimiliki jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Youtube na matokeo yake huwa ni channel yako kufungiwa au kupelekwa mahakamani.
Kuna Aina Nyingi Za Kuingiza Pesa Kupitia YouTube Channel.
1. Google Adsense
Hii Ni Program Ya Google Wenyewe, Wana Kitengo Chao Cha Matangazo Kinaitwa Google Adwords (Hata Wewe Kama Una Biashara Yako Unaweza Kutangaza Pia), Kwahiyo Wafanyabiashara Wanapotangaza Kupitia Hiyo Program, Hayo Matangazo Unaweza Kuyafanya Yakawa Yanaonekana Kwenye YouTube Channel Yako Kupitia Setting (Utaona Kuna Kisehemu Kimeandikwa Monetize Your Account).
2.Direct Ads
Hata Inatokea Kama Channel Yako Imekuwa Maarufu Sana ( Eg Diamond Platnumz & AyoTv ) Na Inatazamwa Na Watu Wengi Zaidi, So Makampuni Yanaweza Kutangazwa Kupitia Channel Yako Directly, Mfano. VodaCom Wanatangaza Directly Kwenye AyoTV Na Diamond Alipata Direct Ad Kutoka Kwa Dr Mwaka
3.Affiliate Marketing
Hii Mara Nyingi Ni Kwa Wale Ambao Hutengeza Tutorials, Unaweza Kufundisha Watu Kufanya Make Up, Then Ukawapa Direct Link Ya Amazon Ya Hizo Bidhaa Unazotumia, Wakizinunua Unapata Commission
N.B.Hakikisha Video Ni Zako Na Ni Quality, Na Si Za Ubaguzi Au Ngono
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link