NEW UPDATES

Idadi ya operesheni alizofanyiwa tundu lissu


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameeleza kuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu, amefanyiwa upasuaji mara 14 na bado ataendelea kufanyiwa kwa mara nyingine ndani ya wiki mbili zijazo.

Mbowe ameyaeleza hayo  alipohudhuria mazishi ya baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda, Wilaya ya Babati Vijijini, mkoani Manyara.

Alisema kuwa licha ya Lissu kuwa ameumizwa vibaya kutokana na shambulio la risasi alilolipata, lakini hali yake imezidi kuimarika na madaktari wanafanya jitihada kubwa ya kuendelea kumuhudumia.

Aliongeza kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwa Lissu kuwepo hai mpaka leo, na ni matumaini yao kuwa baada ya muda Mungu atamponya na kumrdisha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa.

Share :

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link