NEW UPDATES

WEST HAM YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU YA UINGEREZA.


Goli la Pedro Obiang lilikuwa muhimu kwa West Ham ambao walikuwa wanalihitaji ili kuwafanya kuibuka na ushindi wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Huddersfield.

West Ham ambao kocha wao Slaven Bilic alikuwa kwenye shinikizo baada ya kufungwa michezo mitatu, walikuwa chini ya kiwango hata hivyo wageni Huddersfield hawakuwa tishio.

West Ham walipata goli la kwanza katika dakika ya 72, wakati Obiang alipoachia shuti lililomgonga mgongoni Mathias Jorgensen na kumshinda kipa Jonas Lossl, Ayew akaongeza la pili.

                          Pedro Obiang akiangalia shuti lake alilopiga likienda kujaa wavuni


                             Andrew Ayew akiurukia mpira na kuupiga kupachika goli la pili

Share :

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link