Raisi Jacob zuma wa Afrika kusini aelezea alivyonusurika kuuawa kwa sumu.
RAIS JACOB ZUMA WA AFRIKA KUSINI AELEZEA ALIVYONUSURIKA KUUAWA KWA SUMU
Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma kwa mara ya kwanza amezungumzia mbele ya kadamnasi kuhusu majaribio ya kutaka kumuua na kusema kwamba alilinusurika kufa baada ya kuwekewa sumu kwa sababu ya msimamo wake kuhusu masuala ya kijamii, kiuchumi na mabadiliko ya umiliki ardhi nchini humo.
“Nilipewa sumu na nilinusurika kifo kwa sababu Afrika Kusini ilijiunga na Muungano wa Kibiashara wa nchi za Brics (unayojumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini) chini ya uongozi wangu, walisema naipeleka nchi pabaya,” alisema Rais Zuma.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, Rais Zuma aliwaambia wajumbe wa Baraza la Uongozi la chama chake cha ANC mwezi Novemba kwamba yamefanyika majaribio matatu ya kumuua kwa sumu.
Moja ya majaribio hayo lilifanywa na mkewe Nompumelelo Ntuli mwaka 2014 ambalo lilipelekea kwenda nchini Urusi kwa ajili ya matibabu. Baada ya tukio hili, Ntuli-Zuma alifukuzwa katika kasri la Rais Zuma lililopo Nkandla lakini baadaye alikana shutuma hizo.
Addressing hundreds of supporters in Phongolo in the north of KwaZulu-Natal, Zuma said he had become a target for calling for radical economic transformation.
“Kwakuwa tumepigania uhuru, kwanini tusipambane kupata uhuru kamili? Tunashambuliwa kwa sababu tunataka uhuru wa kiuchumi,” alisema Zuma.
Mkutano huu wa makada wa ANC ndio wa kwanza kwa Rais Zuma kuhutubia tangu avuke kikwazo cha Bunge kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye na kushinda wiki iliyopita.
Alisema kuwa chama cha ANC itumie katiba yake kuwapa adhabu kali wabunge wote wa chama hicho walioungana na wapinzani kupiga kura ya kutaka kumuondoa madarakani.
Amesema kwamba anaona ni bora wabunge hawa wafukuzwe uanachama kwakuwa wamefanya kinyume na matakwa ya Katiba ya chama cha ANC.
“Ndio sababu kubwa nataka Katiba ya ANC ifanye kazi. Kwa wale wenye misimamo miwili waache nafasi (ndani ya Bunge) ili zijazwe na wale wenye msimamo mmoja tu wa ANC.
“Tunahitaji umoja ndani ya ANC ambapo maamuzi yakipitishwa, wanachama wote wa ANC wanafata maamuzi hayo,” alisema. Rais Zuma amedai kwamba jaribio la kumuondoa kwa kutokuwa na imani naye ulikuwa ni mpango wa kukiondoa chama chake cha ANC kutoka kwenye uongozi wa nchi hiyo.
Share :
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link