NEW UPDATES

FREEMASONS YAITAHADHIRISHA TANZANIA

FREEMASONS YAITAHADHARISHA TANZANIA

Jumuiya ya Freemasons imeutahadharisha umma wa watanzania kuhusiana na taarifa pamoja na matangazo mbalimbali yanayochapishwa kuelezea namna ya kuweza kujiunga nao.

Katika taarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo, ilieleza kuwa wao hawahusiania na mtu, watu au kikundi cha watu wanaochapisha taarifa hizo kwa lengo la kutawafuta wananchama.

“Jumuiya ya Freemasons Tanzania inayotambuliwa na Jumuiya ya Freemasons Uingereza (United Grand Lodge of England) inapenda kutoa taarifa ya tahadhari kwa umma kuwa kumekuwepo na matangazo ya aina mbalimbali yanayotolewa na watu wasio na uhusiano wowote na Jumuiya hii.”

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa “Tunaufahamisha umma kuwa Jumuiya ya Freemasons haihusiki wala haihusiani na mtu, watu au kikundi chochote kinachotangaza kwa lengo la kutafuta wananchama.”

Inasemekana kuwa watu mbalimbali wamekuwa wakitapeliwa fedha zao kwa ahadi kwamba watasaidiwa kujiunga na jumuiya hiyo ambayo kazi zake halisi hazifahamiki kinabagaubaga.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kwamba hadi sasa hawajapokea malalamiko yoyote yanayohusiana na watu kutepaliwa kwa lengo la kupewa uanachama wa Freemasons na kwamba wakipata malalamiko hayo, watachukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.

Aidha, katika taarifa hiyo, Freemansons wameeleza kwamba hawachukui fedha kwa mtu au watu au kuchukua malipo mengine yoyote kwa mtu anayetaka kuwa mwanachama.

“Jumuiya ya Freemasons Tanzania haitahusika wala kuchukua dhamana kwa mtu au watu watakaotoa fedha au malipo mengine yoyote kwa lengo la kupata uanachama,” ilieleza taarifa hiyo.

Share :

No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link