NEW UPDATES

VANESSA MDEE AWAKOMESHA WALIOKUWA WANAMSEMA JUX

5 hrs ago  Entertaiment

Mwanamuziki Juma Jux ukipenda muite African Boy, leo amehitimu masomo yake nchini China ambapo ametunukiwa Shahada ya Awali (Bachelor Degree) katika masomo ya Sayansi ya Kompyuta (Computer Science) kutoka Chuo Kikuu cha Guangdong nchini China.

Kwa muda mrefu watu mbalimbali wamekuwa wakihoji kuwa Jux anafanya nini China huku wengine wakidiriki kusema kuwa alikuwa akijihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa sababu hawakuwahi kuona hata picha yake akiwa darasani ili kuthibitisha aliyokuwa akiyasema kuwa anasoma.

Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram, Jux amesema kuwa katika miaka minne aliyokuwa akisoma alikumbana na vikwazo vingi ambavyo vilikaribia kumkatisha tamaa lakini baadhi ya watu walimtia moyo na leo amehitimu.

Mbali na Jux, mpenzi wake, Vanessa Mdee ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akimsifia kuwa afadhali amemaliza na picha zake sasa zimeonekana kwa sababu watu walikuwa wakiuliza maswali mengi kuwa anafanya nini China.

“Congratulations @juma_jux U finally done  and you done did it well. Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha.”

Mbali na hilo, Vanessa amempongeza Jux kwa kufanikiwa kufanya kwa pamoja, muziki, biashara na bado akaweza kuzingatia masomo yako jambo ambalo huwashinda watu wengi.

“Umeweza kufanya yote, MZIKI, BIASHARA NA SHULE… now that’s exceptional. Muda wa vibunda babaaa. Keep inspiring the YUTEEEEE 

Hapa chini ni baadhi ya picha za Jux katika mahafali hayo.


No comments

https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link