SIMBA ZIDI YA KAGERA SUGER HUKO BUKOBA
MONDAY, APRIL 3, 2017
HIVI NDIVYO SIMBA ILIVYOPOTEZA MCHEZO WAKE DHIDI YA KAGERA SUGER HUKO BUKOBA
Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa jumla ya bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu bara ambapo baadhi ya wachambuzi wa soka wamesema kuwa kutokana na Kagera Sugar kuifunga Simba inawezekana ikawa ndiyo nafasi kwa yanga kutetea ubingwa wao ambapo baada ya mchezo wa leo Simba wamebaki na pointi zao 55 huku Yanga wakijikita kileleni wakiwa na pointi 56 baada ya michezo 25.
katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba ulishuhudia timu ya soka ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph Huku bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la kufutia machozi kwa Simba sports Club likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi cha pili.
Kwa matokoe hayo yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 56 wakifuatiw ana Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na Azam wenye pointi 44.
Zacharia Hans Poppe akiwa hana hamu baada ya kushuhudia Timu ya Simba ikinyukwa bao 2-1 na Timu ya Wanankurukumbi Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kagera Sugar leo hii jumapili.
Kikosi cha Simba kilichoanza
Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haamini kilichotokea baada ya timu yake kufungwa bao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu bara uliopigwa uwnaja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kichuya Akiambaa na Mpira
Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude akitafakari baada ya timu yake kuchapwa bao 2-1 na Kagera Sugar.
Winga wa timu ya Simba Shiza Kichuya akiambaa na mpira wakati mchezo ukiendelea
Bakihotnews.blogsport.com at Monday, April 03, 2017
No comments:
Bakihotnews.blogspot.com
No comments
https://instagram.com/bakihotnews?utm_medium=copy_link